• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya ukuaji wa uchumi wa China yaendelea kuwa nzuri

    (GMT+08:00) 2017-12-14 17:36:01

    Msemaji wa Idara kuu ya Takwimu ya China Bw. Mao Shengyong leo hapa Beijing amesema, hali ya ukuaji wa uchumi wa China imeendelea kuwa nzuri katika mwezi uliopita, mahitaji ya uzalishaji yanaongezeka kwa utulivu, huku kiwango cha bei za bidhaa kikidumisha utulivu kwa jumla. Wakati huo huo juhudi za kuboresha muundo wa uchumi zinapiga hatua mfululizo, na sifa na ufanisi wa uchumi vinaongezeka siku hadi siku.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Idara kuu ya Takwimu ya China, katika muundo wa sekta za uchumi, uzalishaji wa sekta ya viwanda umeendelea kwa utulivu, hali ambayo imeleta ongezeko la haraka la faida za makampuni, sekta ya huduma imekua kwa haraka, huku kiwango cha ustawi wa shughuli za kibiashara kikiinuka zaidi. Wakati huohuo, uwekezaji kwenye mali zisizohamika umetulia, thamani ya mauzo ya rejereja imeongezeka kwa kasi zaidi, na thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje imekua kwa haraka sana. Msemaji wa Idara kuu ya Takwimu ya China Bw. Mao Shengyong anasema,

    "Katika sekta za uchumi, Sekta ya viwanda nchini China inaelekea kiwango cha kati na cha juu, kwani mwezi Novemba thamani za shughuli za teknolojia ya juu na uzalishaji wa mitambo ya kisasa zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 10 na 14. Wakati huohuo sekta ya huduma za kisasa hasa huduma kwa uzalishaji na mambo ya sayansi na teknolojia, pia inaongezeka kwa haraka, na kudumisha mwelekeo mzuri wa ukuaji. Katika mahitaji ya ndani, thamani ya mauzo ya rejareja imeendelea kukua kwa asilimia zaidi ya 10, ongezeko la mauzo ya bidhaa halisi kupitia mtandao wa Internet likidumisha asilimia 27, huku mauzo ya huduma kupitia tovuti yakiongezeka kwa zaidi ya asilimia 50. Aidha muundo wa uwekezaji pia umeendelea kuboreshwa, wakati kasi ya jumla ya ongezeko la uwekezaji imepungua polepole, uwekezaji unaohusu mambo ya maisha ya wananchi, uvumbuzi wa teknolojia, teknolojia ya hali ya juu na sekta zilizobaki nyuma kimaendeleo nchini China, unaongezeka kwa haraka sana."

    Jambo linalostahili kufuatiliwa ni kupungua kwa kasi ya ongezeko la uwekezaji katika mali zisizohamishika. Kuanzia mwezi Januari hadi Novemba mwaka huu, uwekezaji huo kote nchini China umeongezeka kwa asilimia 7.2. Bw. Mao anaona kuwa kutokana na mabadiliko ya injini za ukuaji wa uchumi, kupungua kwa kasi ya uwekezaji katika mali zisizohamishika huenda hakutaathiri ukuaji wa uchumi. Anasema,

    "Katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya wananchi yanachangia zaidi ya asilimia 60 kwa ongezeko la uchumi. Katika robo tatu zilizopita za mwaka huu, mchango wa matumizi hayo kwa thamani ya uzalishaji mali nchini China ni asilimia 64.5. Hali ambayo imedhihirisha kuwa ukuaji wa uchumi wetu unategemea zaidi mauzo badala ya uwekezaji na mauzo katika nchi za nje. Hali kadhalika, muundo wa injini za uchumi pia umebadilika kwa kiasi kikubwa. Katika robo tatu zilizopita, ongezeko la uwekezaji kwenye mali zisizohamishika limekuwa asilimia 7.5, na kupungua kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, lakini wakati huohuo, kasi ya ukuaji wa uchumi iliongezeka kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na mwaka jana."

    Bw. Mao Shengyong amesema mwakani China itadumisha mwelekeo mzuri wa ukuaji wa uchumi. Hivi karibuni Marekani kwa nyakati tofauti imechukua hatua za kupunguza orodha ya uwiano na kodi, huku ikiongeza riba ya mabenki mara tatu mwaka huu. Hatua ambazo zitaleta athari ya kiasi fulani kwa dunia nzima. Bw. Mao Shengyong amesema, China ina haja ya kupunguza zaidi kodi zake. Anasema,

    "Katika miaka ya hivi karibuni, China imeendelea na hatua za kupunguza kodi. Hadi sasa imepunguza kodi za mashirika takriban yuan trilioni mbili, sawa na dola za kimarekani bilioni 303, ili kuhimiza maendeleo ya uchumi. Hata hivyo mashirika nchini China yanaona mzigo wa kodi bado ni mkubwa, hivyo China bado ina haja ya kupunguza zaidi kodi ."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako