• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi 6 na Iran zasisitiza kuunga mkono makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyuklia

  (GMT+08:00) 2017-12-14 18:19:52

  Nchi 6 zinazojishughulikisha na suala la nyuklia la Iran na Iran zimefanya mkutano wa 10 wa tume ya ushirikiano ya makubaliano ya pande zote kuhusu suala la nyuklia la Iran huko Vienna.

  Akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw.Abbas Araqchi amesema ajenda kuu ya mkutano huo ni kuchunguza suala la nyuklia la Iran na ahadi ya Iran, kutatua masuala kwenye ushirikiano wa hivi sasa na kuondoa vikwazo dhidi ya Iran.

  Ujumbe wa China ulisisitiza kuwa China inaunga mkono makubaliano ya pande zote, na kwamba kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano hayo ni muhimu kwa kulinda mfumo wa kutoeneza silaha za nyuklia wa kimataifa na kuhimiza amani na utulivu wa Mashariki ya Kati, kunalingana na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa. China inazisisitiza pande zote za suala la nyuklia la Iran zitekeleze ahadi kwa pamoja, kuendelea kulinda ukamilifu na umuhimu wa makubaliano hayo, kujenga maelewano kwa kupitia utekelezaji wa makubaliano hayo, na kudhibiti na kutatua mgogoro kwa mwafaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako