• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sheria ya maktaba ya umma kuanza kutekelezwa nchini China mwakani

    (GMT+08:00) 2017-12-15 17:39:38

    Sheria ya Maktaba ya Umma ya Jamhuri ya Watu wa China itaanza kutekelezwa tarehe mosi, Januari mwakani. Naibu waziri wa utamaduni wa China Bw. Yang Zhijin amesema, utekelezaji wa sheria hiyo umedhihirisha mwelekeo wa maendeleo ya maktaba ya umma, lengo la kimsingi na jukumu kuu, na kuimarisha uhakikisho na wajibu wa serikali. Ameongeza kuwa sheria hiyo imeweka kanuni katika ujenzi wa miundo, uendeshaji wa huduma, shughuli za elektroniki, na huduma kwa jamii, na itasaidia maktaba ya umma kupata maendeleo ya mfululizo.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Bw. Yang amesema, utekelezaji wa sheria hiyo utahimiza juhudi za kukamilisha zaidi sheria kuhusu shughuli za utamaduni, na kutoa uhakikisho wa kisheria kwa ajili ya kuongeza hali ya kujiamini kitamaduni, na kuijenga China kuwa nchi ya kijamaa yenye nguvu kubwa ya utamaduni. Sheria hiyo pia itahakikisha maktaba za umma zinatoa huduma bora zaidi, na kuhimiza maktaba hizo kupata maendeleo. Aidha, sheria hiyo pia itasaidia kulinda haki ya kimsingi ya utamaduni kwa wananchi wa China. Anasema,

    "Tutakamlisha zaidi mtandao wa huduma za maktaba ya umma, na kuongeza maeneo yanayoweza kufikiwa na huduma hizo kupitia ujenzi wa uwezo wa kielektroniki, huduma za kuhamahama na huduma za kujihudumia. Pia tutaendelea kuongeza ufanisi wa huduma zetu, na kuhamasisha maktaba katika ngazi zote kukamilisha aina zote za huduma, kuvumbua njia ya kutoa huduma, kuboresha mazingira, na kuongeza uwezo wa kutoa huduma bila ya malipo. Kupitia teknolojia za kisasa za kielektroniki na mtandao wa Internet, tutatoa huduma bora na rahisi zaidi kwa wasomaji wetu."

    Hadi sasa China imemaliza kujenga mtandao wa huduma za maktaba unaoweza kufikia miji na vijiji vote. Lakini bado kuna pengo kati ya sehemu tofauti. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2016, wastani wa idadi ya vitabu kwa mtu katika sehemu za mashariki, kati na magharibi ni 0.86, 0.43 na 0.49. Mkurugenzi wa idara ya utamaduni wa umma ya wizara ya utamaduni wa China Bw. Zhang Yongxin amesema, utekelezaji wa sheria kuhusu maktaba ya umma utatoa uhakikisho katika kupunguza pengo hilo. Anasema,

    "Sheria hiyo pia imeagiza kujenga mtandao wa maktaba za umma katika ngazi sita za taifa, mkoa, mji, wilaya, tarafa na kijiji. Na inatutaka tutumie vya kutosha vifaa vilivyoko tayari katika maktaba za umma, na kuupatia umma bure huduma za kujisomea habari, kuazima vitabu, kutoa semina, uenezaji wa vitabu, kutoa mafunzo na maonesho. Aidha imeagiza kujenga mfumo wa tawi kuu la maktaba ya umma katika wilaya, kuimarisha ushirikiano kati ya maktaba ya umma na maktaba za shule, vyuo, na taasisi ya utafiti wa sayansi, na kuhimiza maktaba za umma kuingiza huduma zake mashinani, ili kuongeza ufanisi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako