• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IMF yasifu makampuni ya China kwa kuisaidia Ethiopia

  (GMT+08:00) 2017-12-15 18:32:37

  Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bi. Christine Lagarde jana amekagua Eneo la Viwanda la Dongfang nchini Ethiopia na kuyasifu makampuni ya China kwa kutoa mchango kwa maendeleo ya huko.

  Eneo hilo lililoko kilomita 40 kutoka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ni eneo la ngazi ya taifa la ushirikiano wa biashara na uchumi la China nchini Ethiopia. Bi. Lagarde amesema, makampuni ya China yamewekeza nchini Ethiopia na kutoa nafasi nyingi za ajira, kusaidia kuinua uwezo wa ufundi wa wafanyakazi wenyeji, na kutoa misaada mikubwa kwa maendeleo endelevu ya biashara na nchi za nje na mageuzi ya uchumi ya Ethiopia. Pia amesema reli kutoka Addis Ababa hadi Djibouti iliyojengwa na kampuni ya China na bandari mpya ya Djibouti zitasaidia maendeleo ya biashara ya Ethiopia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako