• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yataka UN kuchunguza mauaji ya walinzi wake nchini DRC

    (GMT+08:00) 2017-12-15 19:29:26

    Serikali ya Tanzania imeutaka umoja wa mataifa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu shambulizi dhidi ya askari 14 walinzi wa amani wa Tanzania waliouawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Waziri Mkuu wa Tanzania Bw Kassim Majaliwa amesema hayo akiwaongoza mamia ya watanzania waliokuwa wakitoa heshima za mwisho kwa askari hao, kwenye makao makuu ya jeshi la Tanzania mjini Dar es salaam.

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia ulinzi wa amani Bw Jean Pierre Lacroix amesema kuuawa kwa walinzi hao wa amani ni uhalifu wa kivita, uliofanywa na waasi wanaoona shughuli zao zinatatizwa na walinzi wa amani. Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Bw Antonio Guterres amelaani mauaji hayo na kusema ni uhalifu wa kivita na hayakubaliki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako