• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakutana kujadili uamuzi wa Marekani kuhusu Jerusalem

    (GMT+08:00) 2017-12-18 17:53:26

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wake wa kila mwezi kuhusu Mashariki ya Kati, ajenda kuu ikiwa ni Marekani kuutambua Jerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel.

    Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati Bw. Nickolay Mladenov atatoa ripoti kwenye mkutano huo itakayojumuisha majadiliano ya rasimu ya azimio.

    Ili kujibu hatua ya Marekani, ujumbe wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa umekutana na wajumbe wa Baraza la Usalama kujadili suala la azimio la Baraza hilo linaloweza kuwasilishwa katika siku zijazo.

    Wakati huohuo, ndege za kivita za Israel jana usiku zilishambulia kwa makombora maeneo yaliyolengwa ya wapiganaji wa kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza. Shambulizi hilo la Israel lilikuwa ni kujibu mashambulizi ya awali ya makombora yaliyofanyika kutokea Gaza ambayo yaliharibu nyumba mbili lakini hakuna majeraha yaliyoripotiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako