• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasukuma mbele hali mpya ya kufungua mlango kwa pande zote

    (GMT+08:00) 2017-12-19 17:29:30

    Ripoti iliyotolewa kwenye mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China, ilisisitiza kuwa China itaendelea kushikilia sera ya kufungua mlango, na mlango wake utaendelea kuwa wazi zaidi katika siku zijazo. Katika zama mpya China inatakiwa kutekeleza vipi sera hiyo na namna ya kusukuma mbele ufunguaji mlango, limekuwa ni suala linalofuatiliwa sana na wataalamu wa China na wa nje.

    China ikiwa ni nchi inayochukua nafasi ya kwanza na ya pili duniani kwa uuzaji bidhaa na uagizaji bidhaa, na nchi inayoendelea inayovutia kwa wingi zaidi uwekezaji kutoka nje, sera yake hiyo inafuatiliwa sana kwenye jumuiya ya kimataifa. Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya utafiti ya Benki ya Hengfeng Bw. Dong Ximiao anasema,

    "Kufungua mlango kwa pande zote kunahitaji kufanyika kwenye sekta mpya na kwa njia mpya. Sekta mpya, kwa mfano China imetangaza itapunguza vizuizi kwa mashirika ya nje kuwekeza katika hisa, bima, benki na mfuko nchini China. Vizuizi vingi vya zamani vimefutwa au kupunguzwa masharti. Pia kunahitaji njia mpya, yaani kwa sekta za jadi, sasa kuna baadhi ya njia mpya zinazoweza kuvutia uwekezaji kutoka nje na kupanua ufunguaji mlango. Kwa mfano wa kutumia fursa ya "Ukanda mmoja na njia moja", na kuhamasisha makampuni ya China kutumia masoko ya nje, zamani sera ilikuwa inalenga zaidi nchi za Ulaya na Amerika, hivi sasa pia imeongeza nguvu ya kufungua mlango kwa nchi za Afrika na Ulaya ya kati na ya mashariki."

    Wakati wa kufungua mlango zaidi, kujenga eneo la majaribio la biashara huria pia ni moja ya njia mpya zinazojaribiwa. Kampuni ya Ernst & Young ni moja ya makampuni ya huduma ya kimataifa yaliyoingia mapema nchini China, mdau wa huduma za kodi wa kampuni hiyo Bw. Pang Jiade amesema kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, mabadiliko yaliyotokea kwenye soko la China yameinufaisha sana kampuni ya Ernst & Young.

    "Katika miaka kadhaa iliyopita, China imeanzisha eneo la biashara huria, na kuendelea kupunguza vifungu kwenye orodha ya maeneo yaliyopigwa marufuku. Hivi sasa wateja wetu wanaweza kuingia kwenye soko la China kwa uhuru zaidi, na sisi pia tumewezeshwa kutoa huduma bora zaidi, wakati huo huo, tumeona makampuni mengi zaidi ya nje yanaingia China."

    Kuanzisha maeneo ya majaribio ya biashara huria ni mfano mmoja tu wa juhudi za China kutafuta njia mpya za kufungua mlango. Wataalamu wanaona kuwa China pia itatumia fursa ya Ukanda mmoja na njia moja na kurekebisha mfumo wa udhibiti wa orodha ya maeneo yaliyopigwa marufuku, ili kufungua mlango zaidi. Profesa Wang Yifei wa chuo cha mahusiano ya kimataifa cha Chuo kikuu cha Renmin amesema katika zama mpya, kufungua mlango si kama tu kunatokana na mahitaji ya maendeleo ya China yenyewe, na bali pia ni kutafuta ushawishi zaidi kwenye jukwaa la kimataifa.

    "Zamani ufunguaji mlango na mageuzi vilikuwa vinaungana, ili kufungua mlango kwa nje na kufuatana na mwelekeo wa kimataifa, kwa hivyo tuliendelea kurekebisha mifumo ya usimamizi na sheria, hata mawazo ya utendaji. Ufunguaji mlango wa leo unalenga kuongeza nguvu ya ushindani ya mfumo wa China, kufungua mlango si kama tu kunatafuta soko, na bali pia kunainua hadhi na nguvu ya ushawishi wa China, na wa nchi zinazoendelea kwa ujumla, hii ndiyo ni hali mpya tunayodhamiria kujenga."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako