• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ufaransa asema suala la hadhi ya Jerusalemu haliwezi kutengwa  na utatuzi wa mgogoro wa Palestina na Israeli

    (GMT+08:00) 2017-12-20 18:57:27

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema suala la hadhi ya Jerusalemu haliwezi kutengwa na utatuzi kamili wa mgogoro wa Palestina na Israeli.

    Rais Macron amesema hayo jana mjini Paris baada ya kukutana na Mfalme wa Jordani Bw. Abdullah II Bin Hussein aliyeko ziarani nchini Ufaransa. Rais Macron amesema pande hizo mbili zimekubaliana kwamba lengo la kutatua mgogoro wa Palestina na Israeli ni kuanzisha "haki na amani ya kudumu", jambo ambalo ni muhimu katika kudumisha utulivu wa kanda hiyo.

    Pia rais Macron amesema robo ya kwanza ya mwaka ujao itakuwa kipindi muhimu kwa Mashariki ya Kati, na Ufaransa itashirikiana na Jordan katika kuchangia utatuzi wa suala la Palestina na Israel na suala la Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako