• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonyesho ya ajira yanayohudhuriwa na makampuni ya China yatatoa nafasi za ajira elfu moja kwa wanafunzi wa Kenya

  (GMT+08:00) 2017-12-21 18:21:16

  Maonyesho ya ajira yanayohudhuriwa na makampuni ya China yameanza katika chuo kikuu cha Nairobi, na yanatarajiwa kutoa nafasi za ajira elfu 1 kwa wanafunzi wa Kenya, idadi ambayo imeongezeka kutoka mia nne za maonyesho kama hayo ya mwaka jana.

  Mkuu wa taasisi ya Confucious ya Chuo Kikuu cha Nairobi ambacho ni mwandaaji wa maonyesho hayo Guo Hong anasema,

  "Kama tujuavyo, wanafunzi wengi baada ya kuhitimu wanakaa nyumbani kwanza, kwani hawana fursa za kuwasiliana na makampuni mengi kama leo, hivyo tumeandaa maonyesho ya ajira na kuwakutanisha wanafunzi wa kozi mbalimbali na makampuni yenye mahitaji hapa, na kutoa jukwaa hilo kwao."

  Susan Gitau ni msimamizi wa chuo cha ufundi stadi cha Kenya, safari hii amewaongoza wanafunzi zaidi ya hamsini kutoka Thika, mji ulioko umbali wa kilomita 40 nje ya Nairobi, na anaona kuwa maonyesho ya ajira kama hayo yanapaswa kuenezwa ili wanafunzi wengi zaidi wapate fursa za ajira. (sauti 2)

  Mwanafunzi Dennis Obiero kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta ameongozana na wenzake watano kushiriki kwenye maonyesho hayo. Wanavutiwa na baadhi ya kampuni za ujenzi na kutoa maelezo yao.

  Mkuu wa shirikisho la wafanyabiashara la mkoa wa Hunan la Kenya ambaye pia ni meneja wa kampuni ya Arecolor Xu Huanwen ameshiriki kwenye maonyesho hayo mara mbili, na katika maonyesho hayo ya mwaka jana, alipata maelezo zaidi ya 500. Anaona maonyesho ya ajira yanautoa faida kwa makampuni na wanafunzi kwa pamoja.

  "Maonyesho hayo yananufaisha pande mbili. Katika mchakato wa kuhimiza uzawa, makampuni yanaweza kupunguza gharama zao na kuinua ufanisi, huu ni ushindi kwa makampuni. Vilevile, tunawaajiri wanafunzi wazawa, kutoa mafunzo kwao ili waweze kutumia nguvu bora zao, hii imeongeza nafasi za ajira kwa vijana, huu pia ni ushindi kwa jamii ya Kenya."

  Kaimu balozi wa China Li Xuhang ametoa hotuba kwenye maonyesho hayo ya ajira akitoa wito kwa vijana wa Kenya na makampuni ya China kufanya juhudi kwa pamoja ili kujenga siku nzuri za baadaye.

  "China inazidi kuhimiza ushirikiano wa kimataifa, haswa baada ya kutoa pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, uhusiano kati ya China na Kenya umeingia katika enzi ya dhahabu, hivyo nawahamasisha nyinyi vijana kushika vizuri fursa za maendeleo ya China, na pia natarajia makampuni ya China kutumia ipasavyo maonyesho hayo ya ajira, kutafuta vijana wenye vipaji, ili wao na nyinyi makampuni mpate mafanikio kwa pamoja."

  Mkuu wa chuo kikuu cha Nairobi Dkt. Peter Mbithi ameeleza matarajio yake mema na wanafunzi vijana na kutoa shukrani kwa makampuni na mashirika mbalimbali yanayoshiriki kwenye maonyesho hayo. Habari zinasema maonyesho ya ajira ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kenya yatafanyika katika mwezi wa Novemba hadi Disemba kila mwaka katika chuo kikuu cha Nairobi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako