• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Marekani lapitisha muswada wa mageuzi ya kodi

    (GMT+08:00) 2017-12-21 19:14:58

    Bunge la Marekani limeupitisha muswada wa mageuzi ya kodi, ambayo ni makubwa zaidi nchini humo baada ya mwaka 1986. Muswada huo utakaowasilishwa kwa rais Donald Trump wa Marekani kwa ajili ya kusainiwa unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Januari mwaka 2018.

    Kwa mujibu wa muswada huo, kiwango cha kodi ya mapato kwa makampuni kitapunguzwa kutoka 35% hadi 21%. Marekebisho ya kodi kwa makampuni katika muswada huo ni ya kudumu, lakini mabadiliko ya kodi ya mapato kwa watu binafsi yatafanya kazi mpaka mwaka 2025.

    Katika taarifa yake, Rais Trump amesema kwamba mageuzi haya yanalenga kukuza uchumi wa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako