• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Umoja wa mataifa lapitisha azimio kuhusu hadhi ya Jerusalem

  (GMT+08:00) 2017-12-22 09:11:28

  Baraza la umoja wa mataifa limepitisha azimio kuhusu hadhi ya Jerusalem, litakalofanya uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kutambua mji huo kuwa mji mkuu wa Israel usiwe na nguvu ya kisheria.

  Katika kikao cha dharura kisicho cha kawaida, muswada uliowasilishwa na Uturuki na Yemen, umepitishwa kwa kura 128 za ndio 9 za hapana na nchi 35 hazikupiga kura.

  Kabla ya kupiga kura Marekani ilitishia kuwa itakata msaada kwa nchi zitazopiga kura ya ndio na kwa umoja wa mataifa kama azimio hilo likipitishwa.

  Uturuki imekaribisha uamuzi huo, na kusema unatumai kuwa Marekani itabadilisha uamuzi wake bila kuchelewa. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bw. Binali Yildrim amesema azimio hilo limeleta mwanzo mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako