• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Gambia wakutana na kufanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2017-12-22 10:00:47

    Rais Xi Jinping wa China jana amekutana na mwenzake wa Gambia Bw. Adama Barrow ambaye yuko ziara nchini China, kuhusu mustakabali mpya wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Xi Jinping amesema China na Gambia zilirejesha uhusiano wa kibalozi mwezi Machi mwaka jana. Ukweli umethibitisha kuwa uamuzi huo wa Gambia ni sahihi, unaendana na mwelekeo wa maendeleo ya kisasa na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na watu wao.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na Gambia kudumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kwa manufaa ya muda mrefu ya wananchi wao.

    Kwa upande wake rais Barrow amesema kurejesha uhusiano wa kibalozi na China kunaendana na nia ya watu wa Gambia, na Gambia itafuata sera ya kuwepo China moja, kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kuendelea kuimarisha mawasiliano na China katika mambo ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako