• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yatoa maoni kuhusu azimio la kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-12-23 18:50:49

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 23 Disemba, lilipitisha azimio nambari 2397 kutokana na Korea Kaskazini kurusha makombora mwezi Novemba, azimio hilo liliamua kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kwa muafaka. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema kuwa, China inazitaka pande husika zitekeleze kwa usawa maazimio yote ya baraza la usalama kuhusu Korea Kaskazini likiwemo azimio nambari 2397 ili kuhimiza suala la peninsula ya Korea litatuliwe kwa amani.

    Bibi Hua Chunying alisema kuwa, azimio hilo liliimarisha hatua ya vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini na pia lilisisitiza kwamba vikwazo hivyo visiathiri raia wasiokuwa na hatia wa Korea Kaskazini, na visiathiri shughuli na ushirikiano wa uchumi, misaada ya vyakula na misaada ya kibinadamu, visiathiri shughuli za ujumbe wa nchi za nje nchini Korea Kaskazini, alisisitiza kulinda amani na utulivu wa peninsula ya Korea na Asia ya Mashariki na kaskazini, kusisitiza kutatua suala kwa njia ya amani, diplomasia na siasa, kuunga mkono suala la kurudisha mazungumzo ya pande sita, na kuzitaka pande husika kuchukua hatua ili kutuliza hali ya wasiwasi ya peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako