• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya boti kwenye ziwa Tanganyika nchini Tanzania imefikia 19

    (GMT+08:00) 2017-12-25 08:57:38

    Idadi ya watu waliokufa kwenye ajali ya boti iliyotokea kwenye ziwa Tanganyika nchini Tanzania imefikia 19. Ofisa mwandamizi wa idara ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu na majini wa Tanzania SUMATRA Bw. Amaniel Sekulu, amesema miili mingine sita ilipatikana kwenye boti hiyo na kufanya idadi ya watu waliokufa kufikia 19.

    Ajali hiyo ilitokea ijumaa baada ya boti ya MV Atakalo Mola iliyokuwa na abiria 65 kugongana na boti ya MV Pasaka iliyokuwa na abiria 137. Bw Sekulu amesema wengi wa abira wa MV Pasaka walikuwa ni waumini wa kanisa la Pentekoste waliokuwa wanaenda kwenye mkusanyiko wa kusherehekea sikukuu ya Krismas.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako