• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Libya yapanga tarehe ya uchaguzi wa rais na bunge

    (GMT+08:00) 2017-12-25 09:42:31

    Mkuu wa tume ya uchaguzi ya Libya Bw. Imad al-Sayeh amethibitisha kuwa uchaguzi wa rais na bunge utafanyika kabla ya Septemba 30 mwakani.

    Bw. al-Sayeh amesema, mchakato wa kuandikisha wapiga kura unaendelea vizuri, ambapo takriban wapiga kura milioni 1 wamejiandikisha, na idadi hiyo inazidi kuongezeka.

    Mkuu wa tume ya uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Bw. Ghassan Salame mwezi wa Septemba alipendekeza kutekeleza mpango wa kumaliza mgogoro wa kisiasa wa Libya, ambao ni pamoja na kurekebisha makubaliano yaliyopo ya kisiasa ya Libya na kufanya uchaguzi wa rais na bunge. Bw. al-Sayeh amesema, walibya wote wana haki ya kushiriki kwenye uchaguzi huo kama wakiwa na namba ya taifa, huku akithibitisha kuwa waungaji mkono na maofisa wa utawala wa zamani pia wana haki ya kushiriki kwenye uchaguzi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako