• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Tigo ndio mtandao ghali zaidi Tanzania

    (GMT+08:00) 2017-12-25 18:47:27

    Kulingana na ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), kampuni ya mawasiliano ya Tigo ndio inayolipisha wateja wake ada ya juu zaidi kwa kupiga sim,u ba kutuma ujumbe mfupi yaani sms.

    Ripoti hiyo ya robo ya tatu ya mwaka huu inaonyesha kuwa wateja wa mtandao huo hulipa zaidi kuwasiliana kwa namna zote; iwe kupiga au kutuma sms ndani au je ya mtandao au kufanya hivyo nje ya nchi. Kulingana na ripoti hiyo, mwezi wa septemba wateja wa Tigo walitozwa shilingi 360 kupiga simu kwa wenzao wanaotumia mtandao uo huo kwa dakika moja. Hii inafanya mtandao huu kuwa ghali zaidi ikilinganishwa na mitandao mingine. Kwa kawaida, ada ya wastan ambayo hutozwa huwa shilingi 278 kwa dakika.

    Tigo inafuatwa na kampuni ya Vodacom ambayo inalipisha shilingi 270 kwa kila dakika. Inafuatwa na mtandao wa Hatolel kwa gharama ya shilingi 228 kwa dakika kasha Airtel shilingi 219 kwa dakika.

    Wateja wa TTCL wanatozwa shilingi 154 kwa kila dakika, Zantel shilingi 157 na Benson shilingi 60 kwa kila dakika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako