• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makubaliano ya kusimamisha vita yaanza kutekelezwa Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2017-12-25 20:16:58

  Makubaliano ya kusimamisha vita yaliyosainiwa na serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi yameanza kutekelezwa jana, yakiwa na lengo la kurejesha makubaliano ya amani ya mwaka 2015 na kusimamisha vita vya ndani vilivyodumu kwa miaka minne.

  Makubaliano hayo yaliyotolewa na Shirika la Maendeleo kati ya serikali za Afrika ya Mashariki IGAD, yamezitaka pande hizo hasimu kusimamisha operesheni yoyote ya kijeshi na kubaki katika kambi zao na kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa.

  Habari zinasema, rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameuamuru uongozi wa jeshi kufuata makubaliano hayo, huku kiongozi wa kundi kuu la waasi la SPLA-IO Riek Machar akiwataka wafuasi wake kubaki kambini na kuacha mapigano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako