• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Morocco yapata mafanikio makubwa kwenye mapambano dhidi ya ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-12-26 09:24:57

    Morocco imefanikiwa kuvunja vikundi vidogo tisa vya kigaidi kwa mwaka huu, ikiwa ni idadi ndogo ikilinganishwa na miaka michache iliyopita.

    Mwaka 2015 idara za usalama za nchi hiyo zilivunja vikundi 21, mwaka jana zilivunja vikundi 17, na kupungua kwa vikundi hivyo kwa mwaka huu, inaonekana idadi ya vikundi hivyo inazidi kupungua. Idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za ugaidi kwa mwaka huu haijafikia watu 200, wakati katika miaka miwili iliyopita idadi hiyo ilikuwa zaidi ya 275.

    Licha ya mafanikio hayo Idara ya usalama ya Morocco imesema bado kuna tishio la ugaidi, kwani kuna wamorocco waliokuwa wapiganaji wa kundi la IS wanaendelea kurudi nyumbani. Mwaka 2015 wamorocco 92 walikamatwa baada ya kurudi nyumbani, na mwaka huu wamorocco 20 wamekamatwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako