• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajali ya gari yasababisha vifo vya watu 8 na wengine 40 kujeruhiwa Burundi

    (GMT+08:00) 2017-12-26 09:45:12

    Polisi nchini Burundi wamesema ajali ya gari imetokea usiku wa Jumapili kusini mwa Bujumbura, na kusababisha vifo vya abiria wasiopungua 8, na wengine 40 wamejeruhiwa.

    Msemaji wa polisi Bw Pierre Nkurikiye amesema basi la abiria linalomilikiwa na idara ya usafiri wa umma ya Bunrundi, lilikumbwa na ajali katika mkoa wa Rutana, kusini mashariki mwa Burundi, na kupinduka wakati linashuka mlima huko Kamesa, ambapo abiria saba walifariki papo hapo, na majeruhi sita wenye hali mahututi wamekimbizwa hospitali mjini Bujumbura.

    Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa ajali hiyo ilitokana na hitilafu ya breki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako