• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Al- Sisi wa Misri apata saini za milioni 12 wanaounga mkono kugombea muhula wa pili wa urais

    (GMT+08:00) 2017-12-26 09:49:50
    Habari kutoka timu ya kampeni inayomuunga mkono rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri zinasema timu hiyo imekusanya saini za wamisri milioni 12 wanaounga mkono Bw. Al-Sisi kugombea muhula wa pilii wa urais katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2018.
    Hata hivyo Bw. Al-Sisi mwenyewe hajatangaza kama atagombea urais au la, lakini anatarajiwa kupata ushindi mkubwa kutokana na kutokuwepo kwa mpinzani mwenye nguvu.
    Kazi ya kukusanya saini hizo ilianza mwezi Septemba na kufanikiwa kuanzisha makao makuu 168 katika mikoa 27 nchini kote.
    Mratibu mkuu wa shughuli hiyo Bw. Mohamed al-Garhy amesema lengo kuu la shughuli hiyo ni kulinda Misri, akisisitiza kwamba rais Sisi anaweza kulinda nchi hiyo dhidi ya machafuko na mauaji kama yanayoonekana katika nchi nyingine za Kiarabu kama Syria , Libya na Yemen.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako