• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hermas Muvunyi asamehewa

  (GMT+08:00) 2017-12-26 15:17:26

  Kamati ya kitaifa ya Rwanda ya michezo ya olimpiki kwa watu wenye ulemavu NPC-Rwanda imemaliza tofauti zilizojitokeza baina yake na mchezaji wa taifa Hermas Muvunyi na kwamba sasa anaruhusiwa kushiriki baada ya kuomba radhi kutokana na maneno yake kwamba hakuna juhudi za chama hicho au taifa zilizomfikisha katika kiwango alichonacho sasa.

  Kamati hiyo ilimfungia nyota huyo wa kimataifa baada ya mashindano ya olimpiki ya nchini Brazil kufuatia kitendo chake cha kukishutumu chama hicho hadharani kwamba inatoa mchango hafifu katika mashindano ya kimataifa.

  Katibu mkuu wa NPC Dieudonne Mutangana amesema Muvunyi amesamehewa baada ya kutekeleza alichagizwa kufanya na kwamba sasa ataruhusiwa kushiriki mashindano yote na watamuunga mkono kwa asilimia mia moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako