• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wapeleka wasimamizi wa uchaguzi katika marudio ya uchaguzi wa rais nchini Liberia

  (GMT+08:00) 2017-12-26 19:48:01

  Umoja wa Afrika umepeleka wasimamizi wa uchaguzi nchini Liberia wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa marudio ya uchaguzi wa rais unaofanyika leo.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ameidhinishwa kupelekwa tena kwa waangalizi hao ambao wamekuwepo nchini Liberia tangu jumamosi iliyopita na watakuwepo nchini humo mpaka mwisho wa mwezi huu.

  Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na wabunge ilifanyika nchini Liberia Oktoba 10 mwaka huu, na ingawa uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na kwa uwazi, hakuna mgombea aliyepata asilimia 50 inayotakiwa kisheria kuchaguliwa kuwa rais.

  Wagombea wa nafasi ya urais ni rais wa sasa Joseph Boakai wa chama cha Unity na Seneta George Weah wa chama cha CDC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako