• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki yawaua wanachama 7 wa PKK kaskazini mwa Iraq

    (GMT+08:00) 2017-12-27 09:04:09

    Jeshi la Uturuki limesema wanachama saba wa chama cha wafanyakazi wa kikurdi PKK wameuawa kwenye operesheni ya kupambana na ugaidi iliyofanywa na jeshi hilo kaskazini mwa Iraq. Taarifa iliyotolewa na jeshi la Uturuki inasema kwenye operesheni hiyo iliyofanyika kwenye maeneo ya Gara, Metina, Avasin na Basyan nchini Iraq, jeshi hilo lilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya shabaha za wapiganaji wa PKK, ambao wanaaminika kupanga kushambulia vituo vya jeshi la Uturuki. Jeshi la Uturuki lilianza operesheni za kupambana na ugaidi dhidi ya PKK nchini Iraq mwezi Julai mwaka 2015, haswa kwenye eneo la Qandil, ambako ni kambi kuu ya kundi hilo kaskazini mwa Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako