• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji wenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda watungua ndege ya kivita ya Syria katika jimbo la Hama

    (GMT+08:00) 2017-12-27 09:20:29

    Kundi la Nusra Front lenye uhusiano na kundi la Al-Qaeda limeitungua ndege ya kivita ya Syria kwenye jimbo la kaskazini la Hama. Ndege hiyo imetunguliwa ikifanya mashambulizi kwenye maeneo ya kundi hilo.

    Tukio hili limekuja wakati mapambano makali yanaendelea kati ya jeshi la Syria na wapiganaji wa kundi hilo, na baada ya jeshi la serikali kutwaa maeneo kadhaa ya kundi hilo.

    Shirika la habari la Syria SANA limesema operesheni kubwa ya kijeshi kwenye maeneo ya Hama na Idlib imekuwa inaendelea polepole kwa miezi miwili sasa. Lengo la operesheni hiyo ni kutwaa uwanja wa ndege wa kijeshi wa Abu al-Duhur, utakaoliwezesha jeshi la Syria kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya vituo vya kundi la Nursa Front mkoani Idlib.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako