• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza kuu la serikali la Libya laidhinisha rasimu ya sheria ya kura za maoni kwenye katiba

    (GMT+08:00) 2017-12-27 09:35:02

    Baraza kuu la serikali la Libya limeidhinisha rasimu ya sheria ya kura za maoni kuhusu katiba.

    Mjumbe wa baraza hilo Bw Ali Sweih, amesema rasimu hiyo imepitishwa kwenye mkutano muhimu wa baraza hilo uliofanyika jana, na kuhudhuriwa na wajumbe 74, wajumbe 52 kati yao wamepiga kura za ndiyo.

    Ameongeza kuwa mchakato wa upigaji kura umefanyika kwa mujibu wa sura ya 23 ya makubaliano ya kisiasa yanayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa sura hiyo baraza kuu la serikali lenye makao yake mjini Tripoli, na baraza la chini la bunge lenye makao yake mashariki mwa nchi vinatakiwa kuunganishwa katika utungaji wa sheria hiyo ya kura za maoni kwenye katiba pamoja na sheria ya uchaguzi mkuu.

    Lakini bado uamuzi wa baraza kuu la serikali ya Libya, haujakubaliwa na baraza la chini la bunge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako