• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita nchini Jamhuri ya Kongo

    (GMT+08:00) 2017-12-27 09:46:39

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya serikali ya Jamhuri ya Kongo na kundi la upinzani linaloongozwa na Pastor Ntumi.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Stephane Dujarric, inasema katibu mkuu anaelezea matumaini kwamba makubaliano hayo yanasaidia kuleta utatuzi wa amani na endelevu wa vita katika eneo la Pool la nchi hiyo na kupunguza msukosuko wa kibinadamu huko. Eneo la Pool la nchi hiyo ni eneo la kusini linaliozalisha mafuta ikiwa ni pamoja na mji mkuu Brazzaville. Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia pande hizo mbili kutekeleza makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako