• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yaitaka Benki ya Dunia iwe mpatanishi wa kiufundi kuhusu suala la bwawa nchini Ethiopia

    (GMT+08:00) 2017-12-27 09:59:12
    Misri imependekeza Benki ya Dunia kuwa mpatanishi wa kiufundi asiyependelea upande wowote na kutoa uamuzi wa mwisho juu ya mgogoro wa mradi wa Ethiopia wa kujenga bwawa kubwa kwenye mto Nile. Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Misri Bw Ahmed Abu Zeid amesema kwenye taarifa kuwa, mapendekezo hayo yalitolewa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa mambo ya nje wa Misri Bw. Sameh Shoukry, na mwenzake wa Ethiopia Bw. Workneh Gebeyehu. Mkutano huo ulioshirikisha Misri, Ethiopia na Sudan kuhusu bwawa kuu la Ethiopia GERD, haujawa na mafanikio katika mikutano kadhaa iliyopita. Ethiopia na Sudan zinatarajia kupata faida kubwa kutokana na ujenzi wa bwawa hilo huku Misri ikilichukulia hatua hiyo kama ni tishio kutokana matumizi ya pamoja ya maji ya Mto Nile.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako