• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiao kati ya China, Afghanistan na Pakistan haulengi nchi nyingine yoyote

    (GMT+08:00) 2017-12-27 20:20:43

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema kuwa, ushirikiano na mazungumzo kati ya China, Afghanistan na Pakistan haulengi nchi nyingine yoyote, pia hautaingiliwa au kuathiriwa na nchi nyingine.

    Bibi Hua Chunying amesema, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema pande hizo tatu zimekubali kushirikiana kwa pamoja kuhimiza mawasiliano mapana zaidi chini ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Pia kutumia mazungumzo ya usawa ya pande tatu kuthibitisha miradi halisi ya ushirikiano, kutimiza maendeleo na usalama wa pamoja, na kushughulikia amani na utulivu wa kanda hiyo. Amesema mambo hayo yanaendana na mahitaji ya pamoja na maslahi ya pamoja ya nchi hizo tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako