• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 10 wajeruhiwa katika mlipuko St. Petersburg

    (GMT+08:00) 2017-12-28 09:17:01

    Jumla ya watu kumi wamejeruhiwa baada ya mlipuko kutokea jana kwenye supamaketi moja mjini St. Petersburg nchini Russia. Taarifa iliyotolewa na kamati ya kupambana na ugaidi ya Russia, imesema idara hiyo inaratibu operesheni za idara ya huduma za dharura, mamlaka za usalama na idara za kutekeleza sheria, na hatua zinachukuliwa kutafuta wahusika wa uhalifu huo. Kamati ya upelelezi ya nchi hiyo imefungua kesi ya jinai kutokana na tukio hilo, na timu ya uchunguzi inayoshirikisha wataalamu, maofisa kutoka kamati hiyo, Idara ya usalama ya taifa FSB na wizara ya mambo ya ndani, imeanza uchunguzi kuhusu shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako