• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la Sayansi latangaza mafanikio makubwa kumi ya sayansi ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-12-28 09:18:16

    Gazeti la Sayansi limetangaza mafanikio makubwa kumi ya sayansi ya mwaka 2017. Binadamu kushuhudia kwa mara ya kwanza tukio la mawimbi ya mvutano yaliyosababishwa na mgongano kati ya nyota mbili za neutron kumechaguliwa kuwa mafanikio makubwa ya kwanza.

    Mafanikio mengine ni kama yafuatayo:

    Wanasayansi wamegundua aina mpya ya sokwe nchini Indonesia na kumpa jina la Pongo Tapanuliensis baada ya kugundua aina nyingine mpya ya sokwe miaka 90 iliyopita.

    Teknolojia ya hadubini aina ya cryo–electron imewasaidia wanabiolojia kuchunguza vitu vyenye ukubwa wa atomu na kufahamu zaidi molekuli nyingi muhimu kwa viumbe.

    Kutoa tasnifu kwenye mtandao wa Internet kabla ya kujadiliwa na kuidhinishwa na wataalamu kumebadilisha mawasiliano ya kisayansi.

    Wanasayansi wa China wamerekebisha besi iliyobadilika kwenye jeni za mimba ya binadamu.

    Marekani imeidhinisha dawa inayoweza kutibu saratani za aina mbalimbali.

    Wanasayansi wamechimba barafu yenye historia ya miaka milioni 2.7 katika bara la Antaktika.

    Mabaki ya binadamu wa kale yenye historia ya miaka laki 3 yamegunduliwa nchini Morocco.

    Teknolojia za jeni zimefanikiwa kutibu ugonjwa wa misuli unaoweza kurithiwa nchini Marekani.

    Wanasayansi wamechunguza kutawanyika kwa Neutrino kwa kutumia chombo kidogo cha kuchunguza Neutrino.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako