• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Beijing, Tianjin na Hebei zaanza sera ya kuwapitisha wageni bila ya viza ndani ya saa 144

  (GMT+08:00) 2017-12-28 17:40:33

  Kuanzia tarehe 28 mwezi huu, miji ya Beijing na Tianjin na mkoa wa Hebei zitaanza kutekeleza sera ya kuwapitisha wageni bila ya viza ndani ya saa 144. Watu wa nchi 53 wenye vitambulisho vya kimataifa vya kusafiri na tiketi ya kwenda nchi ya tatu wanaweza kuingia au kutoka katika forodha ya sehemu hizo tatu, na kukaa nchini China kwa saa 144 bila ya viza.

  Naibu mkurugenzi wa ofisi ya forodha ya serikali ya Beijing Bw. Zhu Lei leo kwenye mkutano na waandishi wa habari ameeleza utaratibu halisi. Anasema,

  "Wageni wakiwa na vitambulisho vya kimataifa ya kusafiri na tiketi ya ndege ya kwenda nchi ya tatu ndani ya saa 144, wanaweza kuchagua kuingia au kutoka kwenye forodha za Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Beijing, Kituo cha Garimoshi cha Magharibi cha Beijing, Uwanja wa Kimataifa wa Pwani wa Tianjin, Bandari ya Meli za Kimataifa ya Tianjin, Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Shijiazhuang, na Bandari ya Qinhuangdao bila viza. Katika kipindi cha kukaa nchini China, wageni wanatakiwa kujiandikisha ndani ya saa 24 baada ya kupata hoteli, na hawaruhusiwi kutoka nje ya miji ya Beijing, Tianjin na mkoa wa Hebei. Sera hiyo inafaa nchi 53 duniani."

  Nchi hizo ni pamoja na nchi 24 zilizosaini makubaliano ya Schengen zikiwemo Austria, Ufaransa na Ujerumani, nchi 15 nyingine za Ulaya zikiwemo Russia na Uingereza, nchi sita za Amerika, nchi mbili za Oceania, na nchi sita za Asia zikiwemo Korea na Japan.

  Forodha ya Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Beijing ilianza kutekeleza sera ya kuwapitisha wageni kutoka baadhi ya nchi bila ya viza ndani ya saa 72 mwaka 2013. Takwimu zinaonesha kuwa wageni walionufaika na sera hiyo kwa mwaka 2016 walikuwa elfu 26, ambalo ni ongezeko la asilimia 32.2 ikilinganishwa na mwaka 2015. Sera hiyo imekaribishwa na watu wanaotalii au kufanya biashara nchini China. Hata hivyo asilimia 40 ya wageni wanaona muda wa saa 72 hautoshi, hauwezi kukidhi mahitaji ya kufanya utalii na shughuli za biashara, na unapaswa kurefushwa. Hivyo China imeongeza muda huo pamoja na forodha.

  Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya utalii ya mji wa Beijing Bw. Yu Ganqian amesema, mashirika kadhaa ya utalii ya China yamemaliza kutunga mipango ya utalii kwa mujibu wa sera hiyo mpya. Anasema,

  "Kwanza, tumetangaza utamaduni wa China katika matoleo yetu ya utalii kwa wageni. Pili, tumehusisha sehemu zote za Beijing, Tianjin na Hebei. Tatu, tumetoa mipango ya utalii ya kutoka siku moja hadi siku sita, ili kukidhi mahitaji tofauti ya watalii."

  Naibu mkuu wa kituo cha ukaguzi wa forodha cha Beijing Bi Ji Lixia amewakumbusha wageni kuheshimu sheria husika za China wakati wanapotalii nchini China. Anasema,

  "Nataka kukumbusha kuwa, wageni wanaotalii nchini China kutokana na sera hiyo hawawezi kutoka nje ya Beijing, Tianjin na Hebei. Wakiwa na nia ya kutoka sehemu hizo, au kuongeza muda wa kukaa, ni lazima waombe viza kwa idara ya usalama wa umma ya China. Ama sivyo wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria za China."

  Wachambuzi wanaona utekelezaji wa sera hiyo utahimiza maendeleo ya pamoja ya miji ya Beijing na Tianjin pamoja na mkoa wa Hebei, na kusukuma mbele sekta za huduma za sehemu hizo kufungua mlango.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako