• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uturuki atoa mwito wa kuunga mkono mazungumzo ya kitaifa ya Syria

    (GMT+08:00) 2017-12-28 19:25:17

    Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ambaye yuko ziarani nchini Tunisia jana ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mazungumzo ya kitaifa ya Syria yanayopendekezwa na Russia, Uturuki na Iran, ili kuhimiza kutatua suala la Syria kwa njia ya kisiasa.

    Rais Erdogan amesema hayo baada ya kukutana na rais Beji Caid Essibsi wa Tunisia. Amesema, kama rais al-Bashar wa Syria ataendelea kuwa madarakani, usuluhishi wa kimataifa kuhusu suala la Syria hautapata maendeleo yoyote.

    Mazungumzo ya kitaifa ya Syria yamepanga kufanyika mwezi Januari mwaka 2018, mjini Sochi, Russia, kwa lengo la kusukuma mbele mazungumzo ya Geneva kuhusu suala la Syria na mchakato wa amani nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako