• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makamu wawili wa rais wa Zimbabwe waapishwa

  (GMT+08:00) 2017-12-28 19:35:18

  Mkuu wa zamani wa jeshi Constantine Chiwenga na mwanasiasa maarufu Kembo Mohadi wameapishwa kuwa makamu wa rais wa Zimbabwe katika hafla iliyofanyika ikulu ya nchi hiyo mapema leo.

  Makamu hao wa rais waliapishwa na Jaji Mkuu Luke Malaba kufuatia uteuzi wao uliofanywa na rais Emmerson Mnangangwa.

  Bw. Chiwenga aliongoza jeshi kuingilia utawala wa nchi uliosababisha rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe kujiuzulu wadhifa huo mwezi uliopita, na ni moja ya viongozi wa jeshi walioteuliwa na rais Mnangagwa kushika nyadhifa mbalimbali za serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako