• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Morocco yafanikiwa kufanya majaribio ya treni ya kasi

    (GMT+08:00) 2017-12-29 09:23:21

    Shirika la reli la Morocco ONCF limetangaza kuwa Morocco imefanikiwa kufanya majaribio ya treni yenye kasi kubwa zaidi barani Afrika.

    Taarifa iliyotolewa na idara hiyo imesema majaribio yaliyofanyika hivi karibuni yamepata mafanikio, na kasi ya treni imefikia kilomita 320 kwa saa, ikiwa ni tukio muhimu katika historia ya Morocco.

    Katika mwezi Oktoba mwaka huu, majaribio ya treni yenye kasi ya kilomita 275 kwa saa yalifanyika nchini humo, na kushuhudiwa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw Jean-Yves Le Drian.

    Shirika la reli la Morocco pia limesema majaribio yafuatayo yanatarajiwa kufanyika mwezi Februari mwakani kwenye safari nzima kutoka Tangier hadi Casablanca.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako