Serikali ya Zambia inatarajia kupata dola milioni 500 za kimarekani kila mwaka kutokana na mauzo ya tiketi baada ya shirika la ndege la kitaifa litakapoanza kutoa huduma mwaka kesho.
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano Bw. Brian Mushimba amesema sekta ya usafiri wa ndege ya Zambia inahudumiwa na mashirika zaidi ya 10 ya kigeni, yanayosafirisha abiria milioni 1.5 kwa mwaka, lakini nchi yake haikupata faida kutokana na ndege zikikaa kwa muda wa chini ya saa mbili hazitozwi ada.
Aliongeza kuwa kutokana na kurudishwa kwa shirika hilo, serikali inatarajia ongezeko kwenye sekta mbalimbali kama vile utalii, kilimo na uchimbaji madini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |