• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasema njia ya kidiplomasia bado ni njia kuu ya kutatua suala la nyuklia la Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-12-30 16:50:20

    Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis amesema, Marekani inapendelea kutatua suala la nyuklia la Korea Kaskazini kwa njia ya kidiplomasia.

    Bw. Mattis amesema, kwa sasa, Marekani inachukua hatua za kidiplomasia kutatua suala hilo, akitolea mfano, hatua ya waziri wa mambo ya nje ya Marekani Rex Tillerson ambaye atajadiliana na nchi mbalimbali nchini Canada, mwezi ujao kuhusu utatuzi wa suala hilo.

    Pia amesema, muda wa mazoezi ya kijeshi ya muungano ya Marekani na Korea Kusini ya "Foal Eagle" utabadilishwa kutokana na sababu za kisiasa na kidiplomasia.

    Habari zinasema, mwaka huu, Korea Kaskazini imefanya majaribio mengi ya makombora ya nyuklia huku Ikielezwa kuwa Marekani na Korea Kusini zimeendelea kuongeza kiwango cha mazoezi ya kijeshi wakati huu ambapo hali ya peninsula ya Korea ikiendelea kuwa mbaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako