• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi nchini Syria waondoka katika eneo la mwisho walilokuwa wakilishikilia la kusini magharibi mwa Daascus

    (GMT+08:00) 2017-12-30 17:48:42

    Mamia ya waasi pamoja na familia zao ijumaa hii, wameanza kuondoka katika maeneo ya mwisho waliyokuwa wanayashikilia ya kusini magharibi mwa Damascus, na kuelekea katika maeneo yanayokaliwa na waasi ya Kaskazini na Kusini mwa Syria.

    Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ambavyo havikutaka kutajwa majina, walilambia shirika la habari la Xinhua kuwa mabasi yalifika katika kituo cha mjini Saasaa na kuwabeba waasi hao na familia zao kwa ajili ya kuwasafirisha kutoka miji ya Beit Jin, Tal Marwan na Mughor al-Mir kuelekea jimbo la kaskazini magharibi la Idlib pamoja na jimbo la kusini la Daraa.

    Miji hiyo mitatu ndiyo ilikuwa imesalia kwa kukaliwa na waasi wa kundi la Nusra Front lililokuwa na uhusiano na Al-Qaeda katika eneo la Ghuota Magharibi la Damascus.

    Baada ya zoezi hilo la kuondoka kumalizika, ni wazi kuwa eneo zima la magharibi ya Damascus litakuwa huru, kufuatia ya majeshi ya Syria kuwa tayari yameichukua miji ya eneo la Magharibi mwa Damascus.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako