• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yalaumu vikali wanaovuruga makubaliano mapya ya kumaliza mgogoro baina ya pande zinazohasimiana nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-12-30 18:08:20
    Mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Afrika Mashariki IGAD ijumaa hii, amelaani kitendo cha kuvunjika kwa makubaliano yaliyosainiwa na pande zinazohasimiana nchini Sudan Kusini.

    Katika taarifa yake Workneh Gebeyehu, ameeleza masikitiko yake na kuhuzunishwa juu ya kuvurugika kwa makubaliano hayo yaliyosainiwa alhamisi iliyopita mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

    Mwenyekiti huyo pia, amezitaka pande zinazohasimiana kuacha mara moja namna zote za mivutano, na kuwataka wahusika hao kujitafakari juu ya matendo yao.

    Katika taarifa yake pia, amesema kuvunjika tena kwa makubaliano mapya baada ya kusainiwa kunadhoofisha jitihada zinazofanywa na jumuiya ya kimataifa ambayo imeungana pamoja ili kusaidia vyama vya Sudan Kusini kutatua mgogoro kwa njia ya majadiliano jambo litakalosaidia kupatikana suluhu ya kudumu, ili kujenga taifa lao kwa njia ya kidemokrasia.

    Mwenyekiti huyo wa IGAD amesema taasisi hiyo haitaacha kuwachukulia hatua wanaovuruga makubaliano hayo kwa mujibu wa sheria ya kimataifa iliyopitishwa na wakuu wa nchi za IGAD Novemba 24 mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako