• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi awatia moyo wanafunzi wa China wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Moscow na kuwataka wafanye bidii kuzifikia ndoto zao

    (GMT+08:00) 2017-12-31 17:37:48

    Rais Xi Jinping wa China amewashauri wanafunzi kutoka China wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Lomonosov cha mjini Moscow kujitoa kwa ajili ya nchi yao na kufanya kazi kwa bidii ili kuzifikia ndoto zao.

    Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ametoa kauli hizo alipotoa majibu ya barua zilizoandikwa na wanafunzi waliomwandikia ili kueleza uelewa wao juu ya mwelekeo uliotolewa na mkutano wa 19 wa chama cha CPC.

    Amesema nchi itaendelea endapo vijana wake watafanikiwa, nchi itakuwa na matumaini makubwa hapo baadaye iwapo tu itakuwa na vijana wenye mawazo, uwezo na uelewa mkubwa kuhusu uwajibikiaji. Ili kufikia ndoto ya China ya kustawisha taifa, kunahitaji juhudi za vijana, toka kizazi kimoja kwenda kingine.

    Rais Xi pia alitoa salama za mwaka mpya kwa raia wa China wanaosoma nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako