• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Burundi atoa msamaha kwa wafungwa zaidi 2000

    (GMT+08:00) 2018-01-01 08:57:04

    Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 2000 na kuwataka wananchi wake wawe na uzalendo zaidi.

    Kwenye salamu zake za mwaka mpya, rais Nkurunziza amesema wafungwa zaidi 2000 wataachiwa huru katika mwaka 2018, na wanatakiwa kutofanya uhalifu tena.

    Rais Nkurunziza amesema msamaha huo unatolewa chini ya hali ya amani na mshikamano nchini humo, wahalifu watakaosamehewa ni pamoja na wajawazito, wanawake wanaonyonyesha watoto na wale waliohukumiwa kifungo chini ya miaka mitano.

    Pia amewataka wananchi wa Burundi kuchangia pesa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, na kujitokeza kwa wingi kwenye kura za maoni kuhusu katiba zitakazofanyika mwezi Mei mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako