• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfalme wa Morocco ampongeza rais mpya wa Liberia

    (GMT+08:00) 2018-01-01 09:01:10

    Mfalme Mohammed wa sita wa Morocco amempongeza rais mpya wa Liberia Bw George Weah kwa ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu, na kusema Morocco itaimarisha uhusiano kati yake na Liberia.

    Katika ujumbe huo, Mfalme wa Morocco amesema matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha matumaini makubwa ya wananchi wa Liberia katika kuhimiza mpito wa kidemokrasia na kutimiza mustakabali mzuri wa nchi yao.

    Aidha, ameusifu uhusiano wa kirafiki uliopo kati ya nchi hizo mbili, na kusema anapenda kushirikiana na rais wa Liberia kuimarisha uhusiano huo kwenye sekta zote.

    Bw Weah alichaguliwa kuwa rais wa 25 wa Liberia Ijumaa ya wiki iliyopita, na anatarajiwa kuingia madarakani mwezi huu. Ameahidi kuwa ataboresha maisha ya waliberia na kupambana na ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako