• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kombe la Mapinduzi Zanzibar: Azam waanza kwa ushindi

  (GMT+08:00) 2018-01-01 12:16:51

  Mabingwa watetezi Kombe la Mapinduzi, Azam FC wameanza vyema kutetea taji lao baada ya kupata ushindi wa magoli mawili dhidi ya Mwenge FC ya Pemba kwenye mechi iliyofanyika katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

  Magoli ya Azam katika mechi hiyo yote yalifungwa na Paul Peter katika dakika za 41 na 62, na timu hiyo sasa itarejea tena uwanjani Januari 3 kuvaana na Jamhuri ambao nao jana walikuwa na mechi ngumu dhidi ya URA ya Uganda katika mechi za kundi A.

  Michuano hiyo iliyanza rasmi ijumaa iliyopita inaendelea leo hii kwa mechi mbili za kundi B zitakazopigwa katika uwanja wa amani ambapo Mlandege itacheza Zimamoto na JKU watakuwa kibaruani dhidi ya Taifa ya Jang'ombe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako