• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rouhani apinga kauli ya rais Trump kuhusiana na maandamano ya Iran

    (GMT+08:00) 2018-01-01 21:01:40

    Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa hotuba akimkosoa rais Donald Trump wa Marekani kwa kuwahurumia waandamanaji wanaoipinga serikali wa Iran.

    Rais Rouhani amesema, rais Trump ambaye miezi kadhaa iliyopita alidai kuwa Iran inaunga mkono ugaidi ni mtu anayepinga Iran na hana haki ya kutoa maoni kuhusu wananchi wa Iran.

    Akizungumzia maandamano yaliyotokea hivi karibuni katika sehemu mbalimbali nchini Iran, rais Rouhani amesema, wananchi wanaweza kueleza madai yao kwa njia ya amani, kwani kutoa malalamiko na mapendekezo ni haki yao kwa mujibu wa katiba. Lakini malalamiko hayo yanapaswa kusaidia kuboresha mazingira ya nchi na maisha ya raia, na si vitendo vya kimabavu na vinavyoharibu mali ya umma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako