• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utalii kuwa nguzo ya uchumi wa mkoa wa Shanxi nchini China

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:00:49

    Mkoa wa kaskazini wa Shanxi nchini China wenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe, umetoa kanuni za kuanzisha utalii kama nguzo kuu ya ukuaji wa uchumi, ikiwa ni njia ya kujitoa zaidi kwenye sekta ya jadi ya uchimbaji wa makaa ya mawe.

    Kutokana na kanuni hizo zilizoanza kutekelezwa jana, serikali ya mkoa huo itaendeleza sekta ya utalii ili kuwa nguzo kuu ya uchumi kwa kuongeza uwekezaji, kuunga mkono na kuchochea maingiliano na sekta nyingine.

    Mkoa wa Shanxi una historia ya miaka elfu kadhaa, ikiwa na wingi wa mabaki ya kale ya kiutamaduni. Katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Octoba mwaka jana, mkoa huo ulipokea watalii wa ndani karibu milioni 514.8, ikiwa ni ongezeko la asilimia 27 ikilinganishwa na mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako