• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya kisasa kati ya Ethiopia na Djibouti kuanza oparesheni

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:40:46

    Reli ya kisasa inayotumia nishati ya umeme kati ya Ethiopia na Djibouti inatarajiwa kuanza oparesheni rasmi hii karibuni.

    Reli hiyo inatarajiwa kuunganisha maeneo mengi ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili na pia bandari nchini Djibouti.

    Mkuu wa mawasiliano wa shirika la reli la Ethiopia , Dereje Tefera amesema wanafanya matayarisho ya mwisho kabla ya kuanza oparesheni.

    Amesema baadhi ya matayarishi hayo ni kufanyia majaribio ya usimamizi na uendeshaji wa jumla wa treni hiyo.

    Treni ya mizigo itasafiri kwa mwendo wa kilomita 80 huku nayo ile ya abiriria ikisafiri kwa kilomita 120 kwa saa.

    Itakapoanza kazi treni ya mizigo itabeba tani 3,500 kwa wakati mmoja nayo ile ya abiria ikisafirisha watu 2,800 kwa safari moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako