• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Uganda: Rais Museveni ashauri FUFA kutumia vizuri mapato yanayotokana na viingilio

  (GMT+08:00) 2018-01-03 10:08:36

  Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, amelishauri shirikisho la mpira wa miguu la nchi hiyo FUFA, kutumia vyema mapato yanayopatikana kutokana na viingilio vya milangoni kwenye mechi.

  Rais Museveni ameyasema hayo wakati alipokutana na kupata chakula cha mchana na wanamichezo ambapo amesisitiza kuwa yafaa kuwe na bajeti yenye malengo kwa ajili ya kuendeleza soka na timu ya taifa, ambapo amesisitiza kuwa wachezaji wanahitaji matunzo hivyo ni jukumu la FUFA kuhakikisha hilo linatekelezeka.

  Museveni pia ameahidi kuwa serikali itanunua basi jipya kwa ajili ya timu ya taifa ya mpira wa miguu.

  Katika hatua nyingine, amesema serikali imeandaa fedha kwa ajili ya kulipa familia za waathirika wa ajili ya mwaka 2015 baada ya basi lililokuwa limebeba wachezaji wa timu ya taifa kugongana na basi dogo lilikuwa limebeba abiria.

  Takribani shilingi billion moja, fedha za Uganda zimeandaliwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wote waliojeruhiwa katika ajali hiyo pamoja na familia za waliopoteza maisha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako