• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini yapongeza kufunguliwa tena kwa njia ya mawasiliano na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-01-03 17:49:02

    Katibu kiongozi wa rais wa Korea Kusini, Bw. Yoon Young-chan, amesema nchi hiyo imepongeza kufunguliwa tena kwa njia ya mawasiliano na Korea Kaskazini, na kusema ni ishara ya kurejesha majadiliano ya nchi hizo mbili kwa njia ya kawaida.

    Kauli hiyo imetokana na tangazo la Korea Kaskazini mapema leo kuwa itafungua tena kituo cha mawasiliano katika kijiji cha makubaliano ya kusitisha mapigano cha Panmunjom kuanzia saa tisa na nusu alasiri kwa saa za huko.

    Jumanne wiki ijayo, nchi hizo mbili zitafanya majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu masuala mbalimbali, ikiwemo Korea Kaskazini kupeleka washiriki wake katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi itakayofanyika mwezi ujao kwenye kaunti ya Pyeongchan, nchini Korea Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako