• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa kundi la Hamas atoa wito kwa mkakati wa pande zote kukabiliana na hatua za Marekani na Israel kuhusu Jerusalem

    (GMT+08:00) 2018-01-03 17:53:27

    Kiongozi wa kundi la Hamas la Palestina Bw. Ismail Haneya amezitaka pande husika kuweka mkakati wa pande zote wa kukabiliana na hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na Marekani na Israel kuhusu Jerusalem.

    Bw. Haneya amesema, kutokana na msingi wa mapambano yanayoendelea dhidi ya Israel, mkakati huo unatakiwa kuandaa mpango wa pamoja wa wapalestina, nchi za kiarabu na za kiislamu ili kukabiliana na uamuzi wa Jerusalem.

    Pia ametoa wito kwa nchi nyingine zinazounga mkono Palestina na kupinga sera za Marekani katika kanda hiyo kujiunga nao katika mkakati huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako