• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wakaribisha kufunguliwa tena kwa njia ya mawasiliano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2018-01-04 08:45:29

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amekaribisha kufunguliwa tena kwa njia ya mawasiliano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.

    Naibu msemaji wa umoja wa mataifa Bw. Farhan Haq, alisema mazungumzo kati ya pande hizo mbili siku zote ni maendeleo mazuri.

    Bw. Haq amesema katibu mkuu anakaribisha kufunguliwa tena kwa njia ya mawasiliano kati ya wakorea, pia wataendelea na juhudi za kuhakikisha maazimio ya Baraza la Usalama ya kuondoa silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea yanatekelezwa, na kutumai kuwa hatua za kidiplomasia zitaimarishwa ili kuchangia katika kutimiza lengo hilo.

    Kutokana na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya PyeongChang itakayofanyika mwezi Februari mwaka huu nchini Korea Kusini, Korea Kaskazini na Korea Kusini zimefungua tena njia maalumu ya simu katika kijiji cha Panmunjom, zikiwa na matumaini kwa Korea Kaskazini kushiriki kwenye michezo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako