• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia wako hatarini kutokana na mgogoro katika majimbo ya Hama na Idlib

    (GMT+08:00) 2018-01-04 09:45:25

    Shirika la uratibu wa misaada ya kibinadamu la Umoja wa mataifa OCHA limeonyesha wasiwasi kuhusiana na usalama na hali ya maisha ya maelfu ya raia katika majimbo ya kaskazini mashariki mwa Syria ya Hama na Idlib, kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya uhasama.

    Naibu msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Farhan Haq amesema vurugu zilizotokea katika maeneo hayo, zimesababisha vifo na majeruhi kadhaa ya watu.

    Habari pia zinasema, jumanne watu saba waliuawa na wengine 18 walijeruhiwa kutokana na shambulizi la ndege dhidi ya eneo moja la kijijini katika jimbo la Idlib. Katika siku hiyo hiyo watu 25 walijeruhiwa, na maduka na nyumba nyingine kuharibiwa kutokana na mashambulizi ya mizinga. Mashambulizi mengine pia yaliripotiwa katika sehemu mbalimbali za maeneo hayo.

    Umoja wa mataifa umezikumbusha pande zinazopambana kukumbuka wajibu wao kisheria na kuwa makini na usalama wa raia na mali za kiraia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako